Ufafanuzi wa Istilahi Zinazohusiana za Hali ya Hewa

Muhtasari

Nyaraka hii imetoa tafsiri ya ufafanuzi juu ya mpango wa hali ya hewa ya Afrika unaopatikana katika wavuti wa www.africanclimate.net/en/glossary. Tafsiri hii ni katika kwenda sawia na malengo ya mpango wa kueneza ujuzi wa taarifa zinazohusiana za hali ya hewa, kwa watu wa kawaida katika lugha zilizoteuliwa kwa kuwazingatia wao. Kwa ajili ya kurahisisha uelewaji, tumetoa tafsiri nyepesi ya Kiswahili - Kiingereza ya istilahi zilizoteuliwa mwishoni mwa nyaraka, iwapo itahitajika.

Tafsiri

Unasibishaji (Adaptesheni):

Ni uwiano katika mfumo wa vitu asilia au binadamu katika upya au mabadiliko ya mazingira. Unasibishaji katika hali ya hewa hurejelea uwiano katika mfumo wa vitu asilia ua binadamu katika upokezi wa hali halisi au vinayofikiriwa kuwa vichocheo na athari zinazopunguza uharibifu au kutumia fursa zinazofaa

Tathmini Ujinasibishaji (Adaptesheni Asesimenti):

Ni shughuli ya kutambua uwezekano wa kujinasibisha katika mabadiliko ya hali ya hewa na kutathmini kwa kuzingatia kigezo kama cha upatikanaji, faida, gharama, ufaaji pamoja na uwezekano.

Erosoli (Vipandehewa):

Ni mkusanyiko wa hewa kavu au chembechembe zenye unyevunyevu katika kiwango cha sifuri nukta sifuri moja na milimita kumi (0.01 na 10 mm) ambayo huweza kudumu katika angahewa kwa takribani masaa kadhaa. Erosoli huweza kuchagiza halihewa moja kwa moja kupitia kutawanyisha au kufyonza miale na, au siyo moja kwa moja kwa kufanya kama nyukli uevukaji katika utengenezaji wa mawingu au kurekebisha vionwa na kudumu kwa mawingu.

Angahewa (Atmosfia):

Ni gesi ambayo imeizunguka Dunia. Kuna gesi kavu ambayo inajumuisha takribani naitrojeni asilimia sabini na nane nukta moja (78.1%) na oksijeni asilimia ishirini nukta tisa (20.9%) za kiwango cha uwiano wa mchanganyiko pamoja na gesi adimu kama gesi ya argoni yenye asilimia sifuri nukta tisini na tatu (0.93%), heliamu na jopogesi la gesi za mnunurisho (zenye kuathiri hali ya hewa) kama kabonidayoksaidi yenye takribani asilimia sifuri nukta sifuri thelasini na tano (0.035%) na ozoni (hewa ya ozone). Zaidi ya hayo, angahewa inatawaliwa na mvuke ambapo kiwango chake hubadilikabadilika lakini aghalabu huwa asilimia moja (1 %). Angahewa vilevile huwa na mawingu pamoja na erosoli.

Viumbeanuai:

Idadi na uhusiano vinasaba tofautitofauti (asili ya viumbehai), spishi na mifumo ya ekolojia katika eneo fulani mahususi.

Angaviumbe (Bayosfia):

Ni sehemu ya mfumo wa Dunia ambayo inajumuisha mifumo yote ya ekolojia na viumbe hai katika angahewa, ardhi (terestrio angahewa), au katika bahari (bayosfia ya baharini) ikiwemo vyote vitokanavyo na viumbe vilivyokufa (viumbe mfu) kama mboji, udongo utokanao na viumbe vilivyokufa na mabaki ya viumbe wa baharini.

Kechimenti (Eneokitivo):

Ni eneo ambalo hukusanya na kutiririsha maji ya mvua katika sehemu au chanzo kimoja.

Mabadiliko ya Hali ya Hewa:

Ni mabadiliko muhimu ya kitakwimu yanayoelezea hali ya hewa inavyoendelea kwa kipindi cha muda fulani hata wa miaka kumi au zaidi.

Mwitiko wa Hali ya Hewa:

Ni mwingiliano wa utendakazi kati ya michakato katika mfumo wa hali ya hewa. Kwa kawaida, matokeo ya mchakato wa kwanza huzua mabadiliko katika mchakato wa pili ambapo nao huchagiza ama kwa kuuongeza au kuupunguza ule wa awali.

Utathmini wa Matokeo ya Hali ya Hewa:

Ni kitendo cha kutambua na kutathmini madhara na manufaa yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa mfumo wa vitu asilia na kwa binadamu. Miongoni mwa mifumo hiyo huweza kuwa katika sekta ya kilimo, afya, maji, chakula na usalama.

Matokeo ya Hali ya Hewa:

Ni matokeo yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika mfumo wa maumbile asilia na ya binadamu. Kwa kuzingatia hali ya ujinasibishaji mtu anaweza kutofautisha kati ya matokeo ya haraka (yanayowezekana kutukia) na matokeo ya kuchelewa (yale yasiyowezekana kutukia au yanayotukia kwa kuchelewa). Matokeo ya haraka huweza kujitokeza katika hali fulani kwa kila badiliko la utokeaji wa hali ya hewa, bila kuzingatia unasibishaji. Matokeo ya kuchelewa kwa upande mwingine hurejelea matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huja baada ya unasibishaji.

Hali ya Hewa Rejelewa:

Ni uwasilishaji wa mara kwa mara wa mfumo wa hali ya hewa unaozingatia vinavyoonekana, kemikali na vijenzi vya kibailojia, uchangamani wao na mrejesho wa michakato, na kwa kuzingatia vijenzi vyake vyote vinavyofahamika au baadhi yake.

Utabiri wa Hali ya Hewa:

Huu ni ubashiri wa hali ya hewa ijayo ikiwa ni matokeo ya kutaka kutoa ufafanuzi au kukadiria mabadiliko halisi ya jinsi hali ya hewa katika wakati ujao itakavyokuwa. Utabiri huo unaweza kuwa wa msimu fulani, kati ya miaka au katika kipindi kirefu cha kipimo cha muda.

Udhihirikaji wa Hali ya Hewa:

Ni udhihirikaji wa mwenendo wa hali ya hewa katika utawanyikaji ama kwa kuimarika mandhari ya jopogesi na erosoli au mionzi mnunurisho sinario ambapo mara nyingi huzingatia hali ilivyo katika halihewa fulani inayorejelewa. Udhihirikaji wa hali ya hewa unategemea matarajio kuhusu hali ijayo ambayo inaweza au isiweze kutambuliwa katika eneo fulani.

Mandhari ya Hali ya Hewa:

Ni mwelekeo ambao mara nyingi hurahisisha uwasilishaji wa hali ya hewa ijayo kwa kuzingatia mpangilio wa ndani katika uhusiano wa uanahewa ambao umefanywa ili kutumika kwa uwazi katika kuchunguza matokeo muhimu ya mabadiliko ya awali ya hali ya hewa. Mandhari huwa yamejengwa kutokana na mchomozo wa hali ya hewa na mara nyingi hutumika kama mkondo wa tokeo la kurejelewa.

Hali ya Hewa:

Ni ufafanuzi wa kitakwimu kuhusu hali ya hewa (halijoto, mvua, hewa, mgandamizo n.k) unaozingatia wastani wa ubadilikaji wa viwango vinavyohusiana katika kipindi kirefu cha kutoka miezi hadi miaka kadhaa au hata milioni ya miaka. Muda mahususi ambao umefafanuliwa na Jumuiya ya Ulimwengu ya Upimaji wa hali ya hewa (WMO) ni miaka thelasini (miaka 30).

Ukame:

Ni hali inayojitokeza wakati ambapo usimbishaji asidi katika anga ambao unawezesha kuleta mvua huwa umepungua chini ya viwango vya kawaida vinavyotakiwa, kiasi cha kuvuruga mfumo wa mzunguko wa asili ya maji na hivyo kuathiri uwezo wa mfumo wa uzalishaji katika ardhi.

Uwezo Kiuchumi:

Katika muktadha taaluma ya hali ya hewa, dhana hii hurejelea nafasi ya uwezo wa kiteknolojia katika kupunguza upotevu wa jopogesi (nguvu ya kuboreshaji jopogesi) ambao unaweza kukidhi gharama kwa kutengeneza masoko, kupunguza kuanguka kwa soko au kuongezeka kifedha pamoja na usambazaji wa kiteknolojia.

Mwelekeo Kusini wa Eli Ninyo:

Ni hali inayohusisha angahewa na bahari ikiambatananisha mabadiliko ya mwingiliano wa mkandamizo wa kitropiki na mzunguko katika Bahari ya Hindi na Pasifiki. Wakati Eli Ninyo inapotokea, utapakaaji wa mawimbi ya kitropiki hupungua na badala yake mawimbi ya Kiikweta huimarika na kusababisha halijoto ya maji katika eneo la Indonesia kusambaa kuelekea kusini kufunika maji baridi ya mawimbi ya Peru. Tukio hili huwa na athari kubwa katika pepo, halijoto katika usawa wa bahari pamoja na usimbishaji mvua (utengenezaji wa mvua) katika eneo la tropiki la Pasifiki. Kimsingi hali hii huwa na athari katika eneo lote la Pasifiki na maeneo mengine ya ulimwengu. Kinyume cha Eli Ninyo ni La Ninya.

Upotevu Mandhari:

Ni uwasilishaji wa mara kwa mara wa maendeleo yajayo ya vijenzi ambavyo ni mnunurisho muhimu katika kuzuia mionzi ya jua (mfano ni jopogesi na erosoli) kwa kuzingatia mchanganyiko wa seti ya vijenzi vya ndani vinavyofikiriwa kuhusu misukumo (kama vile idadi ya watu, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, mabadiliko ya kiteknolojia n.k) pamoja na uhusiano wake wa msingi wa misukumo hiyo.

Utowekaji (Emisheni):

Katika muktadha wa mabadiliko ya hali ya hewa, dhana hii hurejelea kupotea kwa gesi zinazozuia mionzijua na au viashiria vyake pamoja na erosoli katika angahewa katika eneo na muda mahususi.

Endemiki:

Kwa kuzingatia afya ya binadamu, huu ni ugonjwa unaojitokeza mara kwa mara katika eneo fulani la kijiografia ambapo umekuwa kwa takribani muda wote (ni ugonjwa wakawaida katika eneo fulani la kijiografia).

Ugonjwa wa Mlipuko (Epidemiki):

Huu ni ugonjwa ambao hutokea kwa ghafla na kuathiri idadi kubwa ya watu. Kwa kawaida ugonjwa wa namna hii husambaa kwa kuambukizana. Vilevile dhana hiyo huweza kuhusishwa na ugonjwa wowote au matukio mengine ya kiafya yanayojitokeza kuambatana na mlipuko huo.

Upotevu wa Virutubishomaji (Eutrofikesheni)

Huu ni mchakato ambapo maji (ya bahari, ziwa, bwawa au mto) hufikia kiwango kikubwa cha upotevu wa virutubisho pamoja na msimu ambao kumekuwa na upotevu mkubwa wa oksijeni.

Uziada wa Tukio la Hali ya Hewa:

Hili ni tukio ambalo hutokea mara chache katika takwimu inayorejelewa sehemu fulani mahsusi. Tukio la ziada kwa kawaida huwa nadra kutokea kati ya asilimia kumi na tisini (10 na 90). Tukio la ziada la hali ya hewa ni wastani wa idadi ya matukio ya hali ya hewa katika kipindi fulani cha muda na kwa kawaida ni wastani ambao umezidi ( ama kwa uchache sana au kwa wingi zaidi).

Uhaba wa Chakula:

Ni hali inayojitokeza wakati ambapo watu wanapungukiwa chakula salama na chenye virutubisho kwa ukuaji wao wa kawaida katika afya ya maisha yao. Hali hii huweza kusababishwa na kutopatikana kwa chakula, kutoweza kugharamia bei ya chakula, kuwepo kwa matatizo katika usambazaji au matumiazi ya chakula yasiyotoshelevu katika ngazi ya familia. Uhaba wa chakula unaweza kuwa wa kudumu, wa msimu au wa mpito tu.

Mzunguko wa Kawaida:

Ni mzunguko na mwenendo wa kawaida kimahebu wa angahewa ya Dunia au bahari. Kwa kawaida mzunguko huo huzingatia mfumo wa mgawanyo wa navi (Navier) pamoja na uhusiano wa joto na vyanzo vingine vya nguvu. Migao hiyo ni msingi kwa programu changamani ya kumpyuta ambayo kwa kawaida hutumiwa kuonesha uhalisi wa angahewa au bahari.

Mzunguko wa Jumla:

Ni kiwango kikubwa cha mwenendo wa angahewa na Bahari ikiwa ni matokeo ya utofauti wa joto katika mzunguko wa Dunia kwa minajili ya kuhifadhi uwiano wa nguvu ya mfumo kwa kusafirisha joto na mwendo kani (momentamu).

Halijoto ya Uso wa Dunia:

Ni eneo lenye kiwango cha ulimwengu cha (a) Halijoto ya mwambao wa Bahari (joto la eneo fulani, mita chache kando ya ile halijoto ya jumla ya eneo zima la maji), b) halijoto ya hewa ya eneo la uso wa dunia hadi takribani mita moja na nusu juu ya ardhi.

Ungezeko la Joto Duniani:

Ni ubainishaji mwenendo wa mionzi iliyochanganyika na gesi za ozoni ambazo zinawakilisha mjumuiko wa athari za nyakati tofauti. Gesi hizi hubakia katika angahewa pamoja na uimara wake katika unyonyaji wa mionzi unaoendelea. Kinachoangaliwa ni makadirio ya muda na athari katika tabaka la gesi katika hali ya hewa kwa wakati huu kuhusiana na kaboni dayoksaidi.

Jopogesi (Gesi Grinihausi):

Ni jumla ya gesi zinaounda halihewa (gesi asilia na zisizo asilia) ambazo zinahusika katika kufyonza na kutoa mionzi katika urefu mahususi wa mawimbi ndani ya spektra ya utoaji mionzi chini ya uso wa Dunia na angahewa. Hali hii husababisha athari katika jopogesi.

Haidrosfia (Mjumuisho wa Maji):

Ni jumla ya mfumo wa hali ya hewa wenye unyevunyevu na eneo la maji kama Bahari, maziwa, mabwawa, mito pamoja na maji chini ya ardhi.

Wananchi Wenyeji (Wananchi Asilia):

Ni watu ambao wahenga wao walikuwa na makazi hapo walipo ambapo watu kutoka tamaduni au asili nyingine (Wageni) wamefika katika mazingira yao na kuwatawala kwa kuwateka, kuweka makazi au namna nyingine ambapo kwa sasa wanaishi katika hali ya ukubalifu na usawa kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kimila kuliko jamii nyingine ambazo kwa sasa ndiyo kwanza zinakutana

Mionzi Umeme (Mionzi Mnunurisho):

Ni mionzi ambayo inatolewa katika uso wa Dunia, angahewa na katika mawingu. Vilevile hufahamika kama mionzi chini ya ardhi au mionzi mirefu ya mawimbi. Mionzi hii hubainika kwa viwango vya urefu wa mawimbi (pia huitwa Spektra) mbele zaidi ya urefu wa mawimbi ya rangi nyekundu kwa sehemu ya kuweza kuonekana kwa spektra.

Utathimini Mwingiliano:

Ni njia ya uchambuzi ambayo inajumuisha matokeo na vielelezo kutoka kwa vinavyoweza kuoneka, vya kibailojia, vya kiuchumi, sayansi ya kijamii pamoja na mwingiliano kati ya vijenzi hivyo. Kimsingi kinachozingatiwa ni kutathmini hadhi na matokeo ya mabadiliko ya mazingira na sera kuyahusu.

Matumizi ya Ardhi:

Ni jumla ya mpangilio na shughuli zinazofanywa na binadamu katika ardhi fulani. Shughuli hizo hufanywa kwa malengo ya kijamii na kiuchumi ambapo ardhi inatumiwa.

Mabadiliko ya Matumizi ya Ardhi:

Ni mabadiliko katika matumizi ya ardhi ambayo yanaweza kuibadili ardhi. Ardhi na ubadilishaji wa matumizi ya ardhi huweza kuwa na matokeo katika Albedo, usimbizaji mvua, vyanzo katika jopogesi au katika hali ya hewa kwa jumla katika eneo fulani au kiulimwengu.

Lithosfia (Tabala la Juu katika Ardhi):

Ni tabaka la juu la Dunia linalojumuisha eneo la nchi kavu na bahari likihusisha vipande vya miamba, baridi, unyumbukaji pamoja na sehemu ya juu ya ardhi. Michakato ya kivolkano ni sehemu ya lithosfia, na tabaka hili halichukuliwi kama sehemu ya mfumo wa hali ya hewa lakini hufanya kama sababu ya msukumo wa nje.

Upunguzwaji (Mitigesheni):

Ni uchangamani wa viumbehai katika kupunguza vyanzo vinavyoharibu jopogesi au kuongeza vinavyoimarisha jopogesi hilo. Upunguzaji wa mabadiliko ya hali ya hewa huweza kuwa kama mwingiliano wa vinasabaawali (antropogeniki) ambavyo hutia msukumo katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Uwezo wa Kiupunguzaji:

Ni miundo na hali za kijamii, kisiasa na kiuchumi ambazo huhitajika katika upunguzaji unaotakiwa (upunguzaji wa vinavyoathiri jopogesi).

Monsuni:

Ni upepo katika mzunguko wa jumla wa angahewa ukiainishwa kwa mwelekeo wa upepo unaoendelea katika msimu na kwa mabadiliko yaliyodhihirika katika mwelekeo kutoka msimu mmoja hadi ule unaofuata. (Monsuni ni pepo za msimu katika Bahari ya Hindi).

Upotevu wa Kaboni Dayoksaidi:

Ni utofauti kati ya vyanzo na utowekaji wa kaboni dayoksaidi katika muda fulani na eneo au mkoa mahususi.

Tabaka la Ozoni:

Statosfia ni tabaka ambalo lina kiasi kikubwa cha ozoni. Tabaka hilo huitwa ozoni na limetapakaa takribani kuanzia kilometa kumi na mbili hadi kilometa arobaini (12km - 40km). Ozone imejengeka na kushamiri zaidi kutoka kilometa takribani ishirini hadi ishirini na tano (20km - 25). Tabaka hili huwa linaharibiwa kutokana na uzalishaji wa kemikali za klorini na bromini ambazo zinasababishwa na shughuli za wanadamu kama shughuli za viwanda.

Ozoni:

Ni gesi tatu za kiatomiki za oksijeni (03) zinatengenezwa katika troposfia kutokana na michakato asilia na kwa kujitengeneza kutokana na kuchangamana kwa kemikali pamoja na gesi nyingine zinazotokana na shughuli za mwanadamu. Troposfia hufanya kama jopogesi (hufanya kazi za kudhibiti mionzi mnunurisho) katika Angastrato. Ozoni hutengenezwa kwa kuchangamana kati ya mionzijua na oksijeni molekyula (02). Ozoni angastrato hufanya kazi ya kudhibiti mionzi katika angastrato. Kwa ujumla angastrato imetawala katika tabaka la ozoni na hivyo kuiharibu ozoni angastrato kutokana na ubadilikaji wa kikemikali unaochagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa huweza kusababisha urujuanimionzi B (Ultraviolet-B) katika usawa wa ardhi.

Uparameta:

Katika urejeleaji hali ya hewa, dhana hiyo humaanisha mbinu za kuwasilisha michakato ambayo haiwezi kutatuliwa kwa mapana kianga au utatuzi wa muda mfupi kwa uhusiano kati ya eneo au wastani wa kiwango cha athari za muda kama vile mstari mdogo wa mizani ya michakato na mwenendo wa mizani mikubwa.

Mabadiliko ya Haraka ya Hali ya Hewa:

Kutokuwepo kwa hali ya umstari katika mfumo wa hali ya hewa huweza kusababisha mabadiliko ya haraka ambayo wakati mwingine huitwa matukio ya ghafla au kustaajabisha. Baadhi ya matukio ya ghafla yanaweza kutabiriwa. Mfano wa matukio hayo ni ujiundaji upya wa mzunguko wa halijoto, deglasiasheni ya haraka au uyeyukaji haraka wa barafu unaosababisha mabadiliko ya haraka katika mzunguko wa kaboni. Baadhi ya mabadiliko hayawezi kutabiriwa wala kutarajiwa. Miongoni mwa hayo ni matokeo ya uimara pamoja na mabadiliko ya haraka nje ya mfumo wa umstari (non linear system).

Uthabiti (Risaliensi):

Ni kiwango cha mabadiliko katika mfumo ambayo huweza kufanyika bila ya kuathiriwa hadhi yake (bila huo mfumo kuathirika kutokana na mabadiliko yanayojitokeza).

Mandhari (Sinario):

Ukubalifu ambao mara nyingi hurahisisha ufafanuzi wa namna hali ijayo inaweza kuwa kwa kuzingatia mwingiliano na mpangilio wa vijenzi vya ndani unaohusu nguvu msingi (kama kiwango cha tekinolojia, gharama ya kiuchumi) pamoja na mahusiano. Mandhari siyo utabiri wala maono na wakati mwingine huweza kuzingatia "usimulizi wa kihistoria." Mandhari huweza kutokana na uchomozaji lakini aghalabu huzingatia taarifa za ziada kutoka katika vyanzo vingine.

Utowekaji (Sinki):

Ni mchakato, shughuli au utendakazi wowote unaopunguza jopogesi, erosoli au ishara za jopogesi kutoka katika angahewa.

Stratosfia (Tabakahewa):

Ni tabaka la juu kabisa katika angahewa. Huwa juu ya troposfia ambapo husambaa kutoka aghalabu kilometa kumi (ikitawala zaidi kutoka kilometa tisa katika latityudi ya juu hadi wastani wa kilometa kumi na sita katika Tropiki (9km-16km)) hadi takribani kilometa hamsini (10km-50km).

Utiririkaji Juukando:

Ni maji ambayo yanasafiri juu ya udondo karibu na mkondo. Maji hayo hutiririka katika mkondo wa bonde ambalo halikutoweka toka wakati wa mvua.

Troposfia (Hewatropo):

Ni sehemu ya chini ya angahewa kutoka katika usawa wa Dunia hadi takribani kilometa kumi (10km) katika latityudi ya kati (aghalabu huelea kutoka kilometa tisa katika latityudi ya juu hadi kilometa kumi na sita katika tropiki) ambapo hali ya mawingu hupatikana. Katika troposfia, Halijoto kwa ujumla hupungua kutegemea urefu (umbali).

Udhaniaji (Usiuhakika):

Ni maelezo ya kiwango ambacho hali yake halisi (thamani yake) (kama vile kuhusu mfumo ujao wa hali ya hewa) haifahamiki. Hali hiyo huweza kutokana na upungufu wa taarifa au kutokuwa na makubaliano kuhusu kinachofahamika au hata kinachoweza kufahamika. Kunaweza kuwa na aina nyingi ya vyanzo, kutoka katika hitilafu ya kidata hadi katika utata wa kufafanua dhana, istilahi au kutofahamika kwa utokeaji wa tabia ya wanadamu. Hali ya kutokuwa na uhakika huweza kuwasilishwa kivipimo (kama kwango cha thamani kikihesabiwa kwa virejelewa kadhaa) au kimaelezo (ikirejelewa maamuzi ya timu ya wataalamu).

Uwezekanaji (Vunerabiliti):

Hiki ni kiwango ambacho mfumo huathirika kwa au hukubali kujinasibisha na, kuruhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo kutofautiana kwa hali ya hewa na uziada. Uwezekanaji ni kazi ya kitabia, kimagnityudi na uchelewaji wa mabadiliko ya hali ya hewa ambapo kwayo, mfumo unajibainisha hali yake na uwezo wake wa kupokea mabadiliko.

Mahitaji Makubwa ya Maji:

Nchi husemwa kuwa ina mahitaji makubwa (uhaba wa maji) ya maji kama kiwango cha maji safi yanayosambazwa kinazidiwa na kiwango cha maji yanayotumiwa kama mahitaji muhimu katika maendeleo. Matumizi yanayozidi asilimia ishirini (20%) ya kiwango kipya cha maji kinachosambazwa hutumiwa kama ishara na dalili ya mahitaji makubwa (uhaba wa maji) ya maji.

Utumizi Bora wa Maji:

Ni ujiundaji wa kaboni katika fotosintesisi kwa kila kiwango cha maji kinachopotea katika usafirishajimvuke. Hali hii huweza kuelezwa kifupi kama wastani wa kaboni fotosintesisi inayojiunda kuwiana na kiwango cha maji kinachopotea katika usafirishwaji wake au katika msingi wa msimu kama wastani wa uzalishaji wa kawaida au shughuli za kilimo kwa kiwango cha maji yanayopatikana.